30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Aolewa na baba yake ili kumkomesha dada

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

UKIAMBIWA duniani kuna mambo, basi kubaliana na hilo. Kuna mengi ya kustaajabisha ila huenda usiamini utakaposikia kwa kuwa tu hujawahi kuyashuhudia kwa macho.

Katika hayo, leo hii makala haya yanakukutanisha na familia ya Travis Fieldgrove, mkazi wa Jimbo la Nebraska nchini Marekani.

Fieldgrove mwenye umri wa miaka 39, alimuoa msichana aitwaye Samantha Kershner (21), ambaye katika kile kinachoweza kukushangaza, ni binti yake kabisa.

Hapo unaweza kujiuliza, ilikuwaje jamaa akaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kisha kufunga ndoa kabisa na mtoto yake huyo? Hii hapa simulizi yao.

Inasemekana kuwa chanzo cha Fieldgrove na Samantha kuwa wapenzi ni binti mwingine wa mwanamume huyo.

Eti watoto hao wa kike walianza kama utani na kisha kujikuta katika upinzani mkali, kila mmoja akitamba kuwa angekuwa wa kwanza kupumzika faragha na baba yao huyo.

Huku Fieldgrove akiwa hajui kinachoendelea, aliingia mtegoni, asijue mabinti zake walikuwa kwenye vita kali ya kulinasa penzi lake.

Bahati kwake, mitego ya Samantha ndiyo iliyomnasa mzee wao huyo na rasmi uhusiano wa kimapenzi ulianza Septemba, mwaka jana.

Hawakutaka kuchelewa, mwezi mmoja baadaye, wawili hao waliamua kuingia kwenye ndoa ili waweze kulifaidi penzi lao vizuri.

Hata hivyo, Fieldgrove na Samantha walikutana na mkono wa sheria Januari, mwaka huu, wakishutumiwa kwa uamuzi wao huo wa kuingia katika uhusiano wakati wakifahamu fika kuwa ni baba na mtoto.

Fieldgrove akiwa na mabinti zake

“Kesi hii inawahusisha watu wawili walioingia katika uhusiano wa kimapenzi, wakijua wazi kuwa ni ndugu wa damu. Kabla ya hapo, walikuwa wakifahamiana kabisa kuwa ni baba na mtoto.

“Fieldgrove hakutajwa katika cheti cha kuzaliwa cha Kershner na kule walikokwenda kufunga ndoa huwa hawapimi damu kabla ya kutoa leseni ya ndoa,” inasomeka taarifa ya polisi baada ya uchunguzi wake.

Sheria ya Marekani inaitaja ndoa ya aina hiyo kuwa ni laana, hivyo ilikuwa ni lazima wahusika wakumbane na adhabu kali kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa wengine.

“… inaonekana kwamba waliamua kufunga ndoa haraka iwezekanavyo baada ya kugundua kuwa kulikuwa na uchunguzi dhidi yao,” inaongeza taarifa hiyo.

Mbele ya maofisa wa polisi, msichana huyo hakuficha, alikiri wazi kuwa ni kweli huyo ni mzee wake na alifanya hivyo ili kumshikisha adabu dada yake, ambaye pia alikuwa akimtaka.

Samantha anasema alimjua baba yake akiwa na umri wa miaka 17 kwa kuwa kwa muda mrefu alikuwa akiishi na mama yake.

Kwa utetezi wake huo, bibiye huyo aliepuka kutupwa gerezani na badala yake alikumbana na kifungo cha nje atakachokitumikia kwa kipindi cha miezi tisa. Kesi yake itasikilizwa Julai 16, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, mambo yalikuwa mabaya kwa baba yake wakati wa usikilizaji wa kesi yao mwezi uliopita, kwani kwa kosa lake la kudanganya katika kiapo cha ndoa, akijua wazi kuwa yeye ni baba mzazi wa msichana huyo, alihukumiwa kwenda jela miaka miwili.

Licha ya kujitetea, akisema haamini kwamba msichana huyo ni mtoto wake, vipimo vya DNA ndivyo vilivyomuumbua baada ya kuonesha kuwa wana uhusiano huo wa damu kwa asilimia zaidi ya 99.

“Siamini kuwa mimi ni baba wa Samantha kwa sababu hakuna jina langu katika cheti chake cha kuzaliwa,” anasema Fieldgrove katika mahojiano yake na polisi.

Nayo taarifa ya chombo cha dola hicho ilikinzana naye, ikisomeka: “Samantha ni binti wa Fieldgrove kwa asilimia 99.999.”

Fieldgrove na Samantha

Lakini sasa, wakati Fieldgrove akisikiliza kesi yake mahakamani, mwanasheria wake, Jeff Loeffler, alisema mteja wake alijisikia vibaya na alitamani jambo hilo lisingetokea.

“Pia ana jeraha ndani ya ubongo. Huwa hafanyi kazi nyingi,” anasema mwanasheria Loeffler na kuutupia lawama uamuzi wa mahakama kumwacha nje bibiye Samantha.

Loeffler anaamini wote, kwa maana ya Fieldgrove na Samantha, ni watu wazima. Hivyo, kilichotokea ni makubaliano ya pande mbili na si kama ilivyo sasa ambapo binti huyo anaonekana kutokuwa na makosa.

Fieldgrove hatakiwi kuwasiliana na binti yake huyo kwa sasa na baada ya mwaka mmoja gerezani, ataimalizia miezi mingine 12 akiwa uraiani, japo atakuwa chini ya uangalizi mkali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles