Na Ramadhan Hassan, Dar es Salaam
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amewataka Wakuu wa Mikoa ambao mikoa yao inalima zao la Pamba kuwa na mashamba darasa ambayo yatawasaidia wakulima kujifunza Kilimo cha kisasa.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Bodi ya Pamba pamoja na wadau wa zao hicho.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara, Shinyanga, Kagera, Katavi, Mwanza na Simiyu.
Pia kuliwaWabunge na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Waziri huyo amesema kwa kuweka mashamba darasa itawasaidia wakulima kuona kwa vitendo na hivyo kuwapa urahisi wa kulima kwa mfano.
“Wakuu wa mikoa wekeni sehemu za pilot ili wakulima waone,”amesema.
Pia, amewataka Wabunge kulisemea zao la Pamba pindi hoja zinapoibuliwa bungeni.
“Naomba pia tusajili wakulima kwa wingi hii itatusaidia kuweka vizuri mikakati yetu,” amesema.