24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ANC YAPATA KIONGOZI MPYA

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI


CHAMA tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), jana kilitarajia kupata mrithi wa Rais Jacob Zuma kama kiongozi wake.

Makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa, alikuwa akiongoza kinyang’anyiro hicho cha kumrithi Zuma dhidi ya waziri wa zamani, Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye mbali ya kuwa mke wa zamani wa Rais Zuma, pia alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Afrika.

Harakati hizo za kutafuta kiongozi zimezua mvutano katika chama na kuna hofu kuwa huenda ANC ikagawanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.

Akizungumza katika mkutano huo jana, Rais Zuma aliyeiongoza ANC kwa muongo mmoja, alisema mustakabali wa chama hicho upo katika tishio la kumeguka na kwamba kuna haja ya kuwa na umoja.

Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura.

Zuma alisema tuhuma kuwa Serikali yake ilishinikizwa na masilahi ya wafanyabiashara zitachunguzwa.

ANC imekuwa ikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.

Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baada ya kuwapo madrakani kwa miaka 23.

Mkutano huo ulikutanaisha wajumbe takriban 5,000 mjini Johannesburg.

Wajumbe pia waliwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles