24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA AZANIA KUBORESHA SEKTA BINAFSI

Na Mwandishi Wetu-DodomaUONGOZI wa Benki ya Azania Limited, umeridhika na namna Serikali ilivyopokea mawazo ya wadau wa sekta binafsi katika mkutano walioshiriki kuuandaa mkoani Dodoma kwa lengo la kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

Katika mkutano huo uliofanyika hivi karibuni na kuongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wafanyabiashara kutoka kampuni mbalimbali za binafsi walieleza changamoto wanazokumbana nazo na kushauri njia mwafaka za kuondokana na changamoto hizo ili kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini.
Akizungumzia hali halisi ya kiuchumi nchini Meneja Mkuu wa Miradi, Uwezeshaji na Viwanda wa benki hiyo, Godwin Seiya, alisema kodi ndiyo inayoendesha nchi hivyo hakuna namna ambayo Serikali itaruhusu ukwepaji kodi, lakini mbali na hayo Serikali imefungua milango ya majadiliano na kuwasikiliza wafanyabiashara mambo yanayowakwaza.

“Lengo letu la msingi kuwepo katika mkutano huu ni kutaka kuhakikisha sekta binafsi zinakuwa karibu na Serikali ili kupatikane nafasi ya kuelezana yale yanayoonekana ni kikwazo katika uwekezaji, kama inavyofahamika kazi ya benki ni kutoa mikopo na kuwezesha kampuni kutimiza malengo yake na kumudu kulipa kodi.
“Hii ni heshima kubwa tumepewa wafanyabiashara, katika mkutano huu kama alivyoeleza Waziri Mpango, ndipo ambapo sehemu ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha itatengenezwa kupitia mawazo yaliyotolewa na wajumbe,” alisema Seiya.

Akihutubia wajumbe katika mkutano huo wa siku moja, Waziri Mpango, alisema Serikali haina tatizo na kubadili mfumo wa kodi kwa sababu kila siku wanatafuta namna nzuri ya kukusanya kodi bila kuwakwaza wafanyabiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles