MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Amini Mwinyimkuu, amesema alikuwa kimya kwa kuwa alitaka atoe wimbo mpya baada ya kukamilisha nyimbo tano kwa mpigo.
“Nilitaka niwe na nyimbo zangu tano mkononi ndio nianze kuachia wimbo mmoja mmoja, kwa sababu nataka kuandaa muziki mzuri ili ukitoka ufanye vizuri katika soko la muziki la ndani na nje.