22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Amina Salum Ali ajitosa urais CCM

Amina Salum AliNa Esther Mbussi, Dar es Salaam
MBIO za kuwani urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeanza kushika kasi,baada ya mwanasiasa mkongwe Amina Salum Ali kutangaza rasmi kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba,mwaka huu.
Amina ambaye alikuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU), nchini Marekani anakuwa mwana CCM na mwanamke wa kwanza kutangaza azma yake hadharani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Amina alitoa vipaumbele vyake muhimu ambayo atavitekeleza endapo atapitishwa na CCM kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alivitaja vipaumbele hivyo, kuwa ni kuinua uchumi, kuongeza mapato, kupambana na rushwa, huduma za jamii kuondoa matabaka ya walionacho na wasio nacho na kudhibiti mapato ili yaendane na matumizi.
“Tunaambiwa uchumi umekua kwa asilimia saba…tunataka ukuwe kwa asilimia 10, hatutaki uchumi wa tatu, kwanini tusifikie wa uchumi wa kwanza.
“Katika hili, nia yangu ni kufanya juhudi maeneo yatakayosaidia kukuza uchumi, ikiwamo kuongeza vitega uchumi vya ndani,” alisema.
Alisema ili kuwa na misingi imara ya uchumi endelevu, kinachotakiwa ni kuwawezesha wananchi wa faidi rasilimali zao, wakiwamo wanawake na vijana.
Akizungumzia kilichomsukuma kugombea urais,alisema historia inaonyesha Tanzania haijawahi kuwa na kiongozi wa juu wa serikalini mwanamke.
Alisema uongozi aliopitia tangu enzi za Afro Shirazi Party (ASP) na nafasi yake AU na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), ameshika ngazi za juu.
“Uadilifu, uwezo na malezi ya CCM katika historia yangu ya uongozi, vinanipa nguvu… nafasi iliyobaki kwangu ni kugombea ni urais.
“Kwa imani na itikadi zangu, nimeona ninao uwezo wa kuifikisha Tanzania mahali na wakati ndiyo huu, naamini naweza kuendesha nchi yetu kwa uadilifu, uzalendo na kujituma.
“Kugombea urais, si jambo la kugombana, ni utaratibu wa chama,lazima mtu achaguliwe, watu wananiuliza huogopi kwa kuwa ni mwanamke, nasema siogopi na sioni tatizo kwa kuwa nina uwezo,” alisema.
Alisema kama wanawake na wanaume watachujwa kwa usawa wa kushindana, basi ni wazi ataonyesha maajabu.
Aliwahi kugombea urais wa Serikali wa Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 2000 na kufanikiwa kuingia hadi nafasi ya tano.
Katika mchujo huo, Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume aliibuka mshindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles