27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Sheria ya Takwimu haiwazuii watafiti’

NBS - 1Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa, amesema Sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 haina lengo la kuzuia taasisi au watu binafsi kufanya utafiti wao nchini ila inalenga kuweka misingi imara ya shughuli za takwimu na utafiti.

Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana alipotoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kutungwa sheria hiyo mpya na Bunge Machi mwaka huu.

Dk. Chuwa alisema kuanzishwa kwa sheria hiyo kunalenga kutoa mwongozo kwa taasisi za Serikali na mashirika mbalimbali yanayotoa takwimu nchini yaweze kuendesha shughuli za ukusanyaji na usambazaji wa takwimu kwa kuzingatia sheria hiyo mpya.
“Sheria hii hailengi kuondoa uhuru wa taasisi nyingine za utafiti kufanya kazi zao, taasisi zote za utafiti zinazotambulika katika sheria zitaendelea kuwa huru katika kufanya utafiti kwa mujibu wa taratibu zao mradi tu zinafuata sheria iliyopo,” alisema Dk. Chuwa.

Alisema mbali na sheria kuanisha kuwa takwimu rasmi ni zile zitakazotolewa na Serikali kwa maana Wizara, Idara na taasisi zake kulingana na vigezo vilivyowekwa na kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu ambayo inatoa msisitizo wa takwimu zinazotolewa na taasisi au mtu binafsi kutambuliwa.

“Kifungu cha 20 cha sheria hii kinaeleza kuwa takwimu zinazotolewa na taasisi nje ya Serikali kwa kukidhi vigezo vya takwimu vilivyowekwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiwamo kuzingatia mbinu za kukokotoa takwimu zitatambuliwa kuwa rasmi na zitatumika katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi,” alisema Dk. Chuwa.

Ufafanuzi huo umetolewa siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutia saini Sheria ya Takwimu na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni za 2015.

Hata hivyo, gazeti la The Washington Post la Marekani limekosoa hatua hiyo likidai kuwa itakwenda kinyume na uwazi na utawala bora.

Katika toleo la Mei 15 la gazeti hilo, mwandishi Karen Attiah ambaye ni mchambuzi na mhariri msaidizi wa kitengo cha dijiti ameitaka Serikali ya Marekani na mashirika ya maendeleo hasa Benki ya Dunia kuimulika Tanzania kwa kupitisha sheria zinazokandamiza uhuru wa habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles