24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Amber Rose, Wiz Khalifa waimarisha penzi lao

wizLOS ANGELES, MAREKANI

MKALI wa hip hop nchini Marekani, Wiz Khalifa na Amber Rose, wameonekana kuimarisha penzi lao baada ya juzi kukutwa mitaani wakiwa na mtoto wao.

Wawili hao walikuwa na uhusiano wa muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye walimpa jina la Sebastian, lakini Septemba mwaka jana waliachana.

Taarifa zilisambaa kwamba wamerudiana baada ya msanii huyo kuachia wimbo wake mpya wa ‘See You Again’, ambapo wimbo huo ulimfanya mwanadada Amber Rose kushindwa kuzuia hisia zake na kuomba warudiane na mpenzi huyo.

Juzi wawili hao walikutwa wakiwa katika mitaa ya jiji la Los Angeles wakiwa na mtoto wao, Sebastian. Kupitia akauti ya Instagram ya mrembo huyo, aliandika: ‘Tunaimarisha uhusiano wetu’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles