26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

AMBER ROSE ATEKWA NA MR. IBU

Amber-and-Mr-IbuMPENZI wa zamani wa Wiz Khalifa, Amber Rose, ameonekana kuvutiwa na mwigizaji kutoka nchini Nigeria,
John Okafor ‘Mr Ibu’ kutokana na filamu yake ya Sugar Daddy.

Filamu hiyo ya Sugar Daddy imefanya vizuri nchini Nigeria, lakini kwa sasa imevuka mipaka ambapo imefika
nchini Marekani na kumgusa mrembo huyo.

Kupitia Instagram, Amber Rose aliweka picha ya msanii huyo na kudai kwamba ni ‘bonge la msanii’ ambaye
anavutiwa naye.

“Mr Ibu, anafanya vizuri, nimependa kile ambacho amekifanya katika filamu ya Sugar Daddy. Amenifanya
nivutiwe na filamu hiyo,” aliandika Amber Rose.

Mrembo huyo kwa sasa inasemekana kuwa amerudi kwenye uhusiano na mpenzi wake wa zamani, Wiz Khalifa,
ambaye alizaa naye mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Sebastian, lakini bado hawajaweka wazi kama
wapo pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles