MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, amesema kwa hatua aliyofikia anapata maumivu
ya tumbo wakati wa kulala kiasi cha kukosa usingizi.
Mrembo huyo anatarajia kupata mtoto wa pili, baadaye Desemba, mwaka huu na mume wake Kanye West, lakini kutokana na hatua ambayo ujauzito wake umefikia, anadai inampa usumbufu mkubwa.
“Natarajia kupata mtoto wa pili hivi karibuni, lakini kwakweli kwa sasa napata maumivu ya tumbo wakati wa kulala, hii ni dalili ya kuwa siku yoyote naweza kupata mtoto.
“Hadi kufikia Desemba 26, tayari nitakuwa na mtoto wa pili, nitakuwa na furaha kubwa kuongeza familia yangu,” alisema Kim.