23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyelawiti wachezaji Uganda awa huru

Chris-MubiruKAMPALA, UGANDA

ALIYEKUWA Meneja wa zamani wa Sports Club Villa ya nchini Uganda, Chris Mubiru, aliyefungwa miezi saba jela kwa kosa la kulawiti wachezaji, ameachiwa huru na Mahakama nchini humo baada ya kuonekana hana hatia.

Inadaiwa kwamba kiongozi huyo alikuwa akiwalawiti wachezaji tangu mwaka 2009, lakini baadhi ya wachezaji walimshtaki baada ya miaka mitatu kupita, ambapo waliomshtaki walikosa ushahidi wa kutosha hali iliyomfanya akate rufaa na kuachiwa huru juzi.

Habari kutoka nchini humo zinasema baada ya kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo, kocha huyo alitakiwa kufungwa miaka 10 na kulipa faini ya pesa za Uganda milioni 50 kwa mtu aliyemshtaki aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Nyanzi.

Mubiru alikuwa katika gereza la Luzira tangu Septemba 2015, kutokana na kosa hilo huku uchunguzi ukiendelea, ila mwanzoni mwa wiki hii Jaji wa Mahakama Kuu jijini Kampala, Wilson Masalu, aliweka wazi kwamba kiongozi huyo hana hatia kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha.

Hata hivyo, Jaji huyo aliwataka watu kutoa taarifa mapema baada ya kufanyiwa vitendo kama hivyo ili kuweza kupata ushahidi kwa muda sahihi.

“Washtaki walifanya kosa, walitoa taarifa mwaka 2013 kwa tukio ambalo lilifanyika 2009, hivyo ilikuwa ngumu kufanikiwa kupata uthibitisho juu ya jambo hilo lililokaa miaka mingi.

“Tukio likitokea linatakiwa kutolewa taarifa mapema kwa wakati huo huo ili wachunguzi wamalize mapema uchunguzi wao,” alisema Masalu.

Mwanasheria wa Mubiru alieleza kwamba mshtaki alikuwa na lengo la kutafuta fedha ila mteja wake hakuwa na kosa lolote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles