22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Witness: Simu inanogesha mapenzi yetu

WITNESS9NA BEATRICE KAIZA

SIMU za mkononi zimekuwa chanzo kikubwa cha kugombana kwa wanandoa na wakati mwingine kuharibu mahusiano yao na hata kuvunja ndoa zao, lakini kwa msanii wa hip hop, Witness Mwaijaga ‘Kibonge Mwepesi’ na mpenzi wake, Ochu Shaggy, ni tofauti kwani wao kutumia simu moja haina tatizo kwao.

Mwanadada huyo ambaye anafanya vizuri muziki wa hip hop, amesema mapenzi ya wasanii wengi hayadumu kwa sababu ya kutoaminiana na kwamba simu zao hufungwa na namba za siri kwa hofu ya kufumaniana kupitia simu.

“Mimi na Ochu tunatumia simu moja na hakuna hata siku moja tuliyogombana kisa simu na nimekuwa shuhuda mkubwa wa wapenzi wengi kuachana kisa simu, mimi nawashauri wapenzi wanaofanyakazi na kuwa pamoja kwa muda mrefu watumie simu moja ili heshima iongezeke katika mapenzi yao,” alisema Witness.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles