21.4 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ali Kiba kumfuata Mnigeria wiki ijayo

ally kibaNA MWANDISHI WETU

STAA wa Bongo Fleva, Ali Kiba, mwezi ujao anatarajiwa kukwea pipa hadi nchini Nigeria kwa ajili ya kufanya kazi na mwanamuziki wa nchi hiyo, Deborah Oluwaseyi ‘Seyi Shay’.

Msanii huyo anayetamba na kibao cha ‘Right Now’, aliwaambia waandishi wa habari jambo hilo wakati alipokuwa akizungumzia ziara yake ya kikazi nchini Tanzania.

“Kwa Tanzania namkubali sana Ali Kiba na Christian Bella,” alisema Seyi Shay. “Nimezungumza na Ali Kiba na kukubaliana tufanye kazi pamoja, anatarajiwa kuja Nigeria, Machi mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo.”

Seyi Shay ni balozi wa Pepsi nchini Nigeria na alikuja Tanzania kwa mwaliko rasmi wa kampuni hiyo nchini na alifanya shoo moja mkoani Mwanza kabla ya kutembelea kiwanda cha Pepsi jijini Dar es Salaam kisha kurudi nchini kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles