27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kanye West aomba msaada wa fedha kwa Zuckerberg

Kanye westNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, amemuomba hadharani mwanzilishi wa akaunti ya Facebook, Mark Zuckerberg, amsaidie fedha.

West amemtaka Zuckerberg awekeze bilioni 1 katika miradi yake, huku mwenyewe akidai kwamba hana rasilimali za kutosha kuendesha miradi hiyo.

Ametoa ombi hilo siku chache tu baada ya kutangaza kwamba ana deni la dola milioni 53, wakati alipokuwa anaitambulisha albamu yake mpya.

Hata hivyo, maofisa wa akaunti ya Facebook, wamesema kwamba hawana la kusema kwa sasa ila ombi hilo wamelisikia.

Jambo la kushangaza ni kwamba, msanii huyo ametumia akaunti ya Twitter ili kuweza kufikisha ujumbe huo kwa Zuckerberg, huku mtandao huo ukiwa unashindana na Facebook.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles