MKALI wa wimbo wa ‘Mwana Dar’, Ali Kiba, amekanusha kufanya wimbo wa ushirikiano na mwanamuziki wa kimataifa kutoka Marekani, Neyo.
Ali Kiba alisema ameshangazwa na taarifa hizo, huku akisisitiza kwamba hakuna jambo hilo, lakini wakishirikiana na msanii huyo litakuwa jambo jema.
Katika hatua nyingine, msanii huyo anatarajiwa kuachia wimbo wake mpya, aliouita ‘Nagharamia’ ambao amemshirikisha Christian Bella.
“Nina mpango wa kuachia ngoma yangu mpya hivi karibuni inayoitwa ‘Nagharamia’ ambao naamini utafika katika nafasi mbalimbali za kimataifa,’’ alimaliza.