28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ali Kiba amjibu Diamond Platnum, kudhamini tamasha la Wasafi

Na Anna Potinus – Dar es salaam



Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba amejibu ombi la msanii mwenzake, Nassib Abdul (Dimond Platinum) la kushiriki kwenye Tamasha la muziki la Wasafi Festival linalotarajiwa kuanza Novemba 24 mwaka huu kwamba hatoweza kushiriki kwa kuwa atakuwa na majukumu ya uzinduzi wa kinywaji chake cha Mofaya atakaoufanya nchi za nje.

Awali Diamond Platinum alimualika Ali Kiba kwenye tamasha hilo akitamani Ali Kiba angekuwepo katika tamasha hilo wakaimba pamoja kwani kwa kufanya hivyo ingeonyesha kukuwa kwa wasanii badala ya kutengeneza bifu wakuze muziki wao na watengeneze fedha kwa ajili ya kulisha familia zao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba leo Novemba 7 ameandika kwamba hatoweza kushiriki kwenye tamasha hilo kutokana na yeye kuwa balozi wa kinywaji hicho.

Hata hivyo ameeleza kwamba yeye na kampuni ya Rosckstar wapo tayari kutoa ushirikiano kwa kampuni ya Wsafi kwa kuwapa udhamini kwenye tamasha hilo.

“Tusingependa kuwaacha hivi hivi, tuko tayari kuwapa ushirikiano wa udhamini katika tamasha lenu kupitia Mofaya Energy drink ili kusukuma mbele gurudumu la sanaa Tanzania na Afrika, uongozi wangu utaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya jambo hili kubwa,” amesema

Baada ya kuweka ujumbe huo watu mbalambali wamempongeza msanii huyo kwa kuandika maneno ya busara na kiungwana kujibu ombi la msanii mwenzake huyo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles