28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BoT yaiongezea ‘kifungo’ Bank M

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeongeza muda wa usimamizi wa Bank M Tanzania kwa siku 60 zaidi baada ya muda wa siku 90 kumalizika bila ufumbuzi.

BoT ilichukua usimamizi wa Bank M kuanzia Agosti 2 mwaka huu, baada ya kubaini kuwa benki hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BoT, ilichukua hatua hiyo ili kuipa nafasi BoT kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

“BoT inapenda kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M haujakamilika, hivyo muda wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku 60 kuanzia Novemba 2 mwaka huu, aidha, BoT inauhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha,” imesema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles