30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Gondwe awaita wawekezaji kuwekeza kwenye muhogo Handeni

Amina Omari, Handeni

Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe, amewatoa hofu wawekezaji wanaotaka kujenga viwanda vya kuchakata na kununua zao la muhogo wilayani humo  kuwa ipo ya kutosha na yenye  ubora unaotakiwa.

Gondwe ameema hayo leo Jumatano Novemba 7, wakati akizungumza na wawekezaji waliofika wilayani humo  kwa nia ya kutaka kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha kusindika bidhaa zitokanazo na zao hilo.

“Wananchi wamehamasika kwa wingi kulima zao hilo huku wakifuata ushauri na maelekezo wanayopewa na maofisa kilimo ili kupata muhogo wenye ubora.

“Nashukuru kuona Handeni ni eneo  muhimu la kuja kuwekeza, pia msiwe na wasiwasi kuhusu ubora wa hii mihogo haina shida na mambo ya  upatikanaji wa umeme, ardhi kwa ajili ya viwanda maeneo yapo na hayana migogoro.

“Handeni kuna mihogo bora na safi kuliko sehemu yoyote Tanzania kwa kuwa ina  ardhi ambayo ina mbolea ya asili ambapo shina moja la muhogo inatoa hadi kilo 10 ukilinganisha na maeneo mengine Tanzania,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,  William Mkufwe, amesema atahakikisha anatoa  ushirikiano kwa wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika halmashauri hiyo ili kuwawezesha wakazi wa Handeni kupata soko la zao hilo kwani ni muda mrefu walikuwa wakitegemea zao moja la mahindi kama zao la biashara.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles