26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Alenga Alize aingia tuzo za Maranatha USA

Texas, Marekani

Mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kiswahili huko Texas, Marekani, Alenga Alize maarufu Alenga The Great, amefanikiwa kuingia kwenye tuzo za Maranatha USA 2021.

Alenga ameweka wazi kuwa yupo kwenye vipengele (categories) tatu kupitia filamu zake, Love or Money na Deception Love kama Mwongozaji Bora wa Filamu za Best Inspiration Film.

Aidha Alenga ametoa utaratibu wa kumpigia kura kupitia tovuti ya
https://maranathaawards.com/usa/ au kwa kugusa link iliyopo kwenye ukurasa wao wa Instagram itakayokupeleka kwenye tovuti ya kupigia kura.

“Hapo kwenye website utaingiza jina lako, email yako na CODE yangu kisha unapiga kura kwenye kitufe cha kupigia kura. CODE ambazo unaweza kunipigia kura andika EE4, GG1, GG3 hapo utakuwa umeniwezesha kushinda hiyo tuzo ambazo zitatolewa Jumamosi ya Agosti 28, huko Baltimore, Maryland USA mwisho wa kupigia kura ni Julai 1, 2021,” amesema Alenga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles