28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Meya ataka watumishi Manispaa Tabora kujitathimini

Na Allan Vicent, Tabora

Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa Tabora Ramadhan Shaban Kapela amewataka Watumishi wote katika halmashauri hiyo kuongeza ufanisi ili utendaji wao ulete tija katika mapato ikiwemo kufuta hati chafu waliyopata.

Alibainisha kuwa mkakati wa halmashauri hiyo kwa mwaka huu wa fedha ni kuongeza mapato na kuhakikisha hoja zote zilizopelekea wapate hati chafu zinafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili zisijirudie tena.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika jana mjini hapa Mstahiki Meya alisema kuwa hati chafu sio sifa nzuri kwa halmashauri kwani inaonesha kuwa baadhi ya watumishi hawatimizi wajibu wao ipasavyo.

Alisisitiza kuwa huu si wakati wa kuchekeana, bali kila mmoja ajitathmini kama anatimiza wajibu wake ipasavyo au la, huku akiwataka kufanya kazi kama timu moja, kuheshimiana, kupendana na kuweka uzalendo mbele kwa manufaa ya wananchi.

“Mkakati tuliojiwekea kwa mwaka huu wa fedha ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato, na kurekebisha kasoro zote za kiutendaji zilizopelekea halmashauri kupata hati chafu ili tusipate hati ya namna hiyo mwakani,”’, alisema.

Mstahiki Meya aliwataka kuiga mfano wa Kituo cha Afya Maili-Tano kilichoko katika manispaa hiyo ambapo watumishi wake wameweza kuongeza ufanisi na kufanikiwa kuongeza mapato kutoka sh laki 8 hadi mil 2 kwa mwezi.

Aidha aliwapongeza wasimamizi wa Kituo Kikuu cha Mabasi
cha mjini hapa kwa kusimamia vizuri zoezi la ukusanyaji mapato na kufanikiwa kuingiza hadi sh 1,500,000 tofauti na mapato ya awali ya sh.1,200,000.

Kuhusu Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kushindwa kutatua kero za barabara, Mstahiki Meya aliwataka madiwani kuwa na subira kwa kuwa suala hilo tayari limeshajadiliwa Bungeni na serikali imeshaagizwa kuongeza bajeti.

Aidha katika kikao hicho jumla ya watumishi 18 wakiwemo Maofisa Watendaji wa kata, Maafisa watumishi ambao wapewa vyeo vya muundo,Afisa habari daraja la pili na Mkuu wa kitengo cha uchaguzi ambao wote watapatiwa barua rasmi  yauthibitisho huo.

Kwa  upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora (DAS) Hammarskjolo Yonaza aliwataka Madiwani wote kuhakikisha wanatetea maslahi ya wananchi wao ikiwemo kuwasilisha kero zao katika vikao hivyo ili ziweze kutatuliwa.

Aidha aliwataka Madiwani kushirikiana na Watendaji wa vijiji na kata zao ili kuweka mazingira yatakayosaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato katika vyanzo vyao ili kuharakisha utekelezaji miradi ya maendeleo katika kata zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles