AL-SHABAB WAVAMIA KAMBI YA MAJESHI YA KENYA NCHINI SOMALIA

0
888

Al-Shabab ya nchini Somalia imesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.

Wamewashambulia wanajeshi hao wa Kenya na kuwauwa takriban wanajeshi 50 katika shambulio lililofanyika katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.

Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here