30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WANAUME WALALAMIKA KUNYIMWA TENDO LA NDOA

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA 

BAADHI ya wanaume mkoani Arusha wametajwa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kisaikolojia na kiuchumi, ikiwamo kunyimwa unyumba na wenza wao.

Taarifa iliyotolewa mjini hapa jana na Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha, Mkaguzi wa Polisi, Happyness Temu, ilisema mwaka jana idadi ya wanaume  wanaolalamika imeongezeka mara mbili ikilinganishwa na mwaka juzi.

Vitendo hivyo vimetajwa kufanywa na baadhi ya wanawake wenye uwezo wa kiuchumi kuwazidi waume zao, ambao wakati mwingine wanatoa uamuzi wa familia bila kuwashirikisha wenzi wao.

Hali hiyo imewafanya wanaume kushindwa kutengua uamuzi au kutoa ushauri wakihofia kuzidiwa kipato.

Temu, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema mwaka 2015 wanaume waliolalamikia kunyanyaswa kisaikolojia na wenza wao walikuwa 34 na mwaka jana 63 ambao ni sawa na asilimia 48.

Mkaguzi huyo wa polisi, alisema mwamko wa watu kutoa malalamiko pindi wanapofanyiwa ukatili umetokana na kuenea kwa elimu inayotolewa na dawati kupitia vyombo vya habari, zikiwamo redio na televisheni.

“Mbali na redio, dawati linatoa elimu kupitia vikao vya wazazi mashuleni katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, hatua hii imesaidia wananchi kujua haki zao mahali pa kuanzia pindi wanaponyanyaswa ndani ya ndoa zao,” alisema.

Temu aliainisha malalamiko ya wanaume wanaofika kwenye dawati lake kuwa ni pamoja na kufanyiwa ukatili wa kisaikolojia na kiuchumi, ikiwamo kunyimwa kushiriki tendo la ndoa vitendo vinavyofanywa na wenza wao ndani ya nyumba.

Aidha wilaya inayoongoza kwa idadi ya wanaume kuripoti kufanyiwa ukatili na wake zao ni Arusha walalamikaji 48, Arumeru wanane, Longido wane, Ngorongoro watatu, Karatu na Monduli mmoja kila moja. 

Aidha katika taarifa hiyo, wanaume wengi hawakufahamu kama wao pia wanaweza kutoa malalamiko yao, kama ilivyo kwa wanawake pindi wanapokutana na ukatili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles