Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam
Beki wa mkongwe wa Azam FC, Aggrey Morris, amefunguka juu ya kustaafu kucheza timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, huku akiwaachia usia mabeki chipukizi kuendeleza pale walipoishia.
Morris amesema anaondoka akiwa anaamini wapo watu wenye uwezo wa kuendeleza pale walipoishia, akiwataja miongoni mwao kuwa, Bakari Mwamnyeto na Abdallah Kheri ‘Sebo’.
Amesema alianza kuitwa timu ya Taifa mwaka 2009 ni wakati sasa wakuachia wengine kama wao walivyoachiwa na anaamini anaicha Stars ikiwa salama katika safu ya ulinzi.