23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Magoti na mwenzake wahukumiwa kulipa fidia

Na Imani Nathaniel, Dar es Salaam

Ofisa wa Programu kutoka LHRC Tito Magoti na mwenzake, Theodory Giyani(36), mtaalamu ww mfumo wa kompyuta, wamehukumiwa kulipa fidia ya Sh milioni 17.3 baada ya kupatikana na hatia ya kuongoza genge la uhalifu.

Hukumu hiyo imetolewa leo, Januari 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega, baada ya washtakiwa hao kukiri mashtaka yao kwa DPP.

Mbali na kulipa fidia, mahakama hiyo, imewahukumu adhabu ya kutokutenda kosa lolote la jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia leo.

Hakimu Mtega alisema, mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao kwa kosa la kuongoza gengea uhalifu.

“Washtakiwa mmetiwa hatiani kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu wa kupangwa, hivyo mnatakiwa kulipa kiasi cha Sh 17, 354,535 kama fidia kwa Serikali,” alisema Hakimu Mtega.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana na wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidia kuwa kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya uamuzi kutokana na washtakiwa kukiri mashtaka yao.

Wakili Kadushi amesema washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu, lakini baada ya kufanya majadiliano na DPP, wamefutiwa mawili na kubakisha shtaka moja ambalo ni kuongoza genge la uhalifu.

Kadushi baada ya kueleza hayo, wakili Simom aliwasomea shtaka wa hao, ambapo kati ya Februari mosi na Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam na  katika maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi Tanzania, mshtakiwa Magoti, Giyani na wenzao ambao hawajafikishwa mahakamani,walishiriki makosa ya uhalifu wa kupanga kwa kumiliki programu za kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kufanya uhalifu na kupelekea kujipatia fedha kiasi cha Sh 17, 354,535.

Washtakiwa hao walikuwa wanatetewa na mawakili , Flugence Massawe, Jebra Kambole na Pasiansi Mlowe, waliiomba mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu kwa sababu ni vijana wadogo na wanategemewa na familia zao na walionyesha ushirikiano tangu siku ya kwanza walipofikishwa mahakamani hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles