23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Afisa Tanesco kortini kwa wizi wa vifaa vya Sh milioni 800

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Afisa Manunuzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Kurasini, Clement Mlai amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Februari 22, mchana akituhumiwa kwa wizi wa vifaa mbalimbali vya umeme vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 800.

Mshtakiwa anakabiliwa na shtaka lingine la kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh 821,387,780 akiwa mwajiriwa.

Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali Mkuu, Martenus Marandu, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu, amedai mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai, 2018 na Juni, 2019.

Mshtakiwa anadaiwa kuiba vifaa mbalimbali vya umeme ukiwemo waya, vyote jumla vikiwa na thamani ya Sh 821,387,780 mali ya Tanesco.

Katika shtaka la pili anadaiwa kulisababishia shirika hasara ya kiasi hicho cha fedha, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu sababu kesi yake ya uhujumu uchumi, amekwenda rumande hadi Machi 8, mwaka huu kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa, upelelezi haujakamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles