Afande Sele: Nikifa nichomwe moto

0
924

Afande SeleNA HERIETH FAUSTINE

MFALME pekee wa rhymes nchini, Afande Sele, ameshangaza mashabiki wake alipodai kwamba akifa maiti yake isizikwe bali ichomwe moto kama baadhi ya madhehebu yanavyofanya.

Afande ambaye kwa sasa amepumzika katika shughuli yake ya muziki kwa muda, aliweka wazi mambo hayo hivi karibuni alipokuwa katika mazungumzo na watangazaji wa kipindi cha Planet Bongo.

“Nikifa nichomwe moto kwa kuwa ninaamini waliochomwa moto hufufuka na kuwa malaika siku za mwisho nami nataka nifufuke nikiwa malaika huko mbinguni, hivyo nataka nikifa nichomwe moto,” alieleza Afande kwa kusisitiza.

“Imani yangu inanituma kuwa nikizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo nitakuwa binadamu jambo ambalo mimi silitaki tena nataka siku ya ufufuo niwe malaika,” alisema Afande Sele.

Katika hatua nyingine, Afande Sele alisisitiza kuhusiana na umuhimu wa kilimo kwa wasanii wanaopata nafasi ya kulima wafanye hivyo kwa kuwa kilimo kina faida.

Baada ya kushindwa kupata nafasi ya ubunge aliyokuwa akigombea Jimbo la Morogoro Mjini, Afande alisema kwa sasa anaendelea na shughuli za kilimo katika mashamba yake yaliyopo Mkuyuni mkoani Morogoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here