33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Adadi ataka mradi wa maji Muheza ukamilike haraka

MWANDISHI WETU-DODOMA

MBUNGE wa Muheza, Balozi Adadi Rajab (CCM), amesema kitendo cha mradi wa maji unaotoa maji kutoka Tanga Pongwe hadi mjini Muheza kutokamilika kwa wakati, kinasababisha kero kubwa kwa wananchi.

Amesema kwamba, mradi huo ulitarajia kukamilika Mei mwaka jana, lakini hadi sasa bado unaendelea kujengwa ingawa hadi sasa umekamilika kwa asilimia 70.

Balozi Adadi aliyasema hayo bungeni jana alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2019/20.

“Kazi kubwa inafanyika, lakini mradi huu ambao tunautegemea, ulikuwa kwenye mpango huo ili kupunguza tatizo la maji Muheza.

“Kwa sasa hivi imebaki kama asilimia 30 ili maji yaanze kutiririka ingawaje hayatakidhi sehemu kubwa.

“Kwa sasa, tatizo lililobaki ni kufumua mabomba yaliyochakaa mjini Muheza na kuweka mapya na suala hilo limesitishwa kidogo kusubiri mradi mkubwa wa maji kutoka nchini India wenye thamani ya Dola za Marekeni milioni 500.

“Tayari nimezungumza na waziri husika kuhusu hilo na kusisitiza aruhusu sasa hivi ili mabomba hayo yaanze kufumuliwa kwa sababu tenki ambalo lilikuwa linachelewesha, limeshatengenezwa na limekaribia kukamilika.

“Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu mmefika pale na mmeona kazi iliyofanyika kwa kutoa tenki kubwa Pongwe na mabomba ya chuma yamelazwa kuelekea kwenye chanzo kikubwa.

“Pamoja na hayo, kwenye bajeti ya wizara nimeona zimetengwa zaidi ya Shilingi milioni 700, hivyo namuomba waziri aruhusu wakati mradi mkubwa unasubiriwa, mabomba hayo yaanze kufumuliwa ili mkandarasi aanze kazi na maji yapatikane wakati wanasubiri mradi huo mkubwa,” alisema Balozi Adadi.

Kuhusu ongezeko la tozo ya maji ya Sh 50, alisema suala hilo limekuwa likipigiwa kelele kwa miaka mitatu sasa na kwamba imependekezwa kuwa tozo hiyo inatakiwa kuongezwa ili kufikia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles