26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuendelea kukarabati vituo vya afya

RAMADHAN HASSAN

SERIKALI imesema itaendelea kukarabati miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kadri upatikanaji wa rasilimali fedha.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini,Seleman Bungara (CUF).

Katika swali lake,Bungara alidai kwamba Hospital ya Wilaya ya Kilwa,haina jokofu la kuhifadhia maiti na pia majengo yake mengi ni chakavu.

“Je,Serikali ina mpango gani wa kununua jokofu jipya sambamba na kukarabati majengo ya Hospitali hiyo,”aliuliza Bungara.

Akijibu,Waitara alisema Hospitali ya Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa Hospitali kongwe nchini na imekuwepo tangu  mwaka 1965.

“Kwa kutambua umuhimu wa hospitali hiyo,Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imekuwa ikifanya ukarabati na upanuzi wa majengo mbalimbali ya kutolea huduma,”alisema.

Alisema mwaka wa fedha 1996 -1997 ukarabati wa miundombinu mbalimbali ulifanyika  pamoja na ujenzi wa kliniki ya mama na mtoto pia mwaka wa fedha 2010 ulifanyika ujenzi wa jingo la huduma za Ukimwi (CTC) na mwaka 2017 ulifanyika ujenzi wa jingo la mama ngojea.

Naibu Waziri Waitara alisema Hospital ya Wilaya ya Kilwa  ina jokofu la kuhifadhia maiti lilonunuliwa mwaka 1996,hivyo lina uwezo  wa kuhifadhi mwili mmoja tu.

Alisema Serikali inaendelea na taratibu za kukamilisha hatua za kuanza ujenzi wa jingo jipya  la kuhifadhia maiti kwenye Hospital hiyo,sambamba na ununuzi wa jokofu jipya la kisasa.

Naibu Waziri huyo alisema Serikali itaendelea kukarabati miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kadri upatikanaji wa rasilimali fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles