25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

AC Milan yamtimua kocha wake

Sinisa MihajlovicMILAN, ITALIA

ALIYEKUWA kocha wa zamani wa Sampdoria, Fiorentina na Serbia, Sinisa Mihajlovic, amefukuzwa kazi na klabu yake ya AC Milan.

Kocha huyo alikuwa anaitumikia klabu hiyo ya AC Milan tangu mwaka jana, lakini kwa sasa amefukuzwa kazi kutokana na timu hiyo kupoteza michezo mitano mfululizo na kuwafanya washike nafasi ya sita katika msimamo wa ligi nchini Italia.

Kufukuzwa kwa kocha huyo kunampa nafasi kocha wa timu ya vijana ya klabu hiyo, Cristian Brocchi, hadi mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo alichukua nafasi ya Filippo Inzaghi, lakini ameshindwa kufanya kile ambacho klabu hiyo kinahitaji hasa kutokana na matokeo mabaya mwishoni mwa wiki iliyopita kocha huyo alijikuta akipokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Juventus.

Klabu hiyo iliweka wazi kwamba imeachana na kocha huyo lakini wanashukuru kwa mchango wake na wanamtakia maisha mema kokote aendako.

“Klabu inaweka wazi kwamba imeachana na kocha wao, Mihajlovic, lakini inamshukuru kwa jitihada zake za kupigania timu na inamtakia mafanikio mema kwenye klabu nyingine ambayo ataipata,” waliandika AC Milan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles