23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Abramovich ataka ushindi Chelsea

Roman Abramovich
Roman Abramovich

LONDON, ENGLAND

MMILIKI wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich, hivi karibuni alikuwa katika   kikao na viongozi wakuu wa klabu hiyo ili kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi katika michezo ijayo.

Abramovich alifanya mazungumzo na bodi ya timu hiyo baada ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka timu ya Liverpool, huku akitaka timu hiyo kutorudia uzembe waliofanya hadi  kupoteza pointi tatu nyumbani.

Bosi huyo alishuhudia kikosi chake chenye thamani ya pauni milioni 117 kikiwa na vipaji lukuki kikicheza chini ya kiwango kwa mara ya kwanza tangu kiwe chini ya kocha, Antonio Conte.

Hata hivyo, kocha huyo hayupo katika presha kubwa tangu awe kocha wa timu hiyo.

Lakini Abramovich alitoa tahadhari timu hiyo kutorudia makosa waliyofanya msimu uliopita ambao walimaliza nafasi ya kumi na kusababisha kumfukuza aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, baada ya kufanya vibaya tangu mwaka 1995-96.

Hata hivyo, kipigo dhidi ya Liverpool kilimshitua kocha wa timu hiyo, Conte, ambaye ulikuwa mchezo wake wa kwanza kupoteza Ligi Kuu England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles