30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 7, 2022

Contact us: [email protected]

Makelele amtabiria makubwa Kante

Claude Makelele
Claude Makelele

LONDON, ENGLAND

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Chelsea, Claude Makelele, amesema ana matumaini ya kumuona beki wa sasa wa timu hiyo, N’Golo Kante, akiwa bora zaidi yake.

Makelele alisema beki huyo ana kazi kubwa ya kufanya kabla ya kuwa bora katika timu hiyo.

Kante anafananishwa na Makelele kutokana na aina ya uchezaji wake, baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea timu ya Leceister City.

Makelele aliwahi kucheza timu ya Real Madrid, Paris Saint-Germain na Marseille, kabla ya ujio Chelsea wa kiungo, Nemanja Matic, ambaye alithibitisha kuwa tayari Kante ni bora zaidi ya Makelele.

Mkongwe huyo anaamini kuwa Kante ni miongoni mwa wachezaji bora katika eneo la ukabaji, lakini alisisitiza anatakiwa kuwa na kiwango bora zaidi.

“Eneo la ukabaji ni eneo ambalo ni gumu kucheza, lakini Kante ni miongoni mwa wachezaji wanaomudu vema eneo hilo.

“Anatakiwa kuwa kiongozi, kila mchezaji anatamani kucheza na Kante, hivyo kutokana na ubora wake huenda akawa bora zaidi yangu ingawa anahitaji muda zaidi kuwa bora,” alisema Makelele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,662FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles