26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Abiria 300 wa boti wanusurika ajali ya moto

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

ABIRIA 300 wamenusurika kufa baada ya Boti ya Royal waliyokuwa wakisafiria kutoka Kisiwa cha Unguja kwenda Pemba baada ya boti hiyo mali ya Kampuni ya Ocean Enterprises kuwaka moto  ikiwa baharini.

Tukio hilo lilitokea nyakati za mchana katika eneo la Matumbini wakati ikielekea kuwasili katika Bandari ya Mkoani, Kisiwani Pemba.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana kutoka Unguja, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Zanzibar, Omar Maalim alisema ajali hiyo ilitokea baada ya kuwapo hitilafu ya umeme katika chumba cha injini na kusababisha kuwaka moto mkubwa.

Hata hivyo, alisema abiria waliokuwamo katika boti hiyo walifanikiwa kuokolewa kwa kuhaulishwa katika boti ya Serengeti ambayo ilikuwa jirani na eneo la tukio.

Kwa mujibu wa Maalim, tayari wametuma wataalamu kisiwani Pemba kwenda kufanya uchunguzi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kubaini chanzo cha ajali hiyo.

“Ukaguzi wetu utaangalia document  za meli iko katika hali gani, chanzo pamoja na bima ya meli na lengo letu si kumkomoa mwekezaji isipokuwa ni kupunguza matukio kama si kuyaondoa kabisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles