27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ujenzi wa shule wakwama kwa zaidi ya miaka mitano, DC na Mbunge waingilia kati

Na Mwandishi Wetu, Biharamlo

Wanafunzi 350 kuanzia darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya Msingi Busiri iliyopo kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo wanalazimika kutumia vyumba viwili vya madarasa kutokana na ujenzi wa vumba hivyo kukwama baada ya wananchi  kugoma kuendelea kuchangia kwa kigezo cha kutojua matumizi ya fedha wanayoichanga.

Wakiwa kwenye ziara ya kusikiliza kero za wananchi jana Desemba 8, mwaka huu, viongozi hao wamefika katika shule hiyo na kujionea halihalisi ya namna wananfunzi hao wanavyosoma huku shule  nzima ikiwa haina madawati na kuwalazimu wanafunzi  hao kukaa chini.

Awali  akitoa taarifa ya shule hiyo  mwalimu mkuu, mwalimu Stephano Raphael amesema kuwa shule hiyo  inazo changamoto nyingi ikiwemo  Madawati, Vyumba vya madarasa,vyoo vya wanafunzi ambapo ameeleza kuwa  wananfunzi hao  wanalazimika  kutumia matundu mawili ya vyoo  hali  inayowapelekea kuishi kwa tabu sana.

Akiongea na wanafunzi pamoja na wwalimu shuleni hapo, mkuu wa wilaya ya Biharamulo Kanali Mathias Kahabi ameupongeza uongozi  wa shule kwa kuendelea kuwafundisha wanafunzi japo  kwa mazingira magumu na kuwaahidi kuwa changamoto hizo  zinakwenda kumalizika muda sio  mrefu.

“Wakati wa kampeini wananchi walimsimamisha Mhe. Waziri mkuu hapa alipokuwa  akitokea Ngara na kumueleza suala la shule hii  ambayo awali ilikuwa na walimu  watatu tena wa kujitolea, maelekezo yalitolewa hapo  hapo na walimu wakaletwa wanne sasa niwaombe wanangu vumilieni kwenye kipindi hiki kifupi hizi changamoto tutazimaliza ndio maana nimekuja hapa pamoja na mbunge.” Amesema Kanali Kahabi.

Katika mkutano wa hadhara na wananchi, Mbunge wa jimbo la Biharamuo Magharibi Mhe. Mhandisi Ezra Chiwelesa amewashukuru wananchi hao kwa kuanzisha ujenzi wa shule hiyo baada ya kuona watoto wao  wakishindwa kusoma kutokana na shule kuwa mbali ya zaidi  ya kilometa 18 na  kuwapelekea watoto hao kukosa muelekeo wa maisha.

Ezra amesema kuwa kijiji hicho ambacho kipo kwenye maeneo  ya machimbo  ya madini   ya Dhahabu haiwezekani wananchi  washindwe kujenga shule kwaajili ya watoto wao na kuwataka wananchi  hao  kueleza tatizo  ni nini  hadi ujenzi umekwama kuendelea.

“Ninyi ni wazazi na wanaotakiwa kusoma hapa ni watoto wenu haiwezekani mkashindwa kuendeleza ujenzi huu, kuna msingi wa vyumba 6 ambao umesimama kwa takribani miaka 5 hebu  tuelezeni shida ni nini? Kama kuna tatizo tumekuja sasa kulimaliza maana watoto wanatia huruma na kwa serikalihiiya awamu  ya 5 hatuwezi kuruhusu hali  hiyo ikaendelea.” Amesema Mbunge Ezra.

Wakitoa kero walizonazo  baadhi wananchi hao wengi wao wamekuwa wakisumbuliwa na migogoro ya ardhi ambayo   imesababishwa na viongozi  wa kijiji hicho kwa kuwanyang’anya ardhi zao na kuwauzia watu wenye fedha huku wengine wakiwa wamedhurumiwa kabisa.

“Tumepoteza watoto wengi hapa hasa wa kike kwa kupata mimba na wengine kuolewa, wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda kutafuta shule na huko wanakutana na watu wanaoedesha masemi ambao wamekuwa wakiwabeba kwa lengo la kuwa lifti na wengine wameishia darasa la nne kwa kushindwa kumu mwendo wa kwenda shuleni zaidi ya kilomita 18” amesema mmoja wa wanakijiji.

Kuhusu mkwamo wa shule wananchi hao wamesema kuwa wamekatishwa tama na viongozi wa kijiji akiwemo mtendaji wa kijiji pamoja na mwenyekiti  wa kijiji kwa kuwachangisha michango ya ujenzi  wa shule bila kuwasomea mapato na matumizi lakini wakihoji wanaambiwa makaratasi ya kumbukumbu ya michango yamepotea.

Alipoulizwa kuhusu suala la kusoma taarifa ya mapato na matumizi mtendaji wa kijiji hicho Omary Ramadhan amejibu kuwa anakumbukumbu za watu   ambao hawajalipa huku mwenyekiti wa kijiji hicho  akisema kuwa kumbukumbu za waliochangia hazipo.

Mara baada ya kusikiliza hoja hizo viongozi   hao waliwatia moyo wananchi  na kuwaeleza kuwa utatengenezwa utaratibu mzuri wa uchangiaji na kuwahakikishia kuwa hakuna pesa yao ambayo italiwa na badala yake itatumika kuwaletea maendeleo ambapo  mkuu  wa wilaya aliamua kuondoka na mwenyekiti pamoja na mtendaji kwaajili ya mahojiano zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles