28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

DAWASA yaibuka mshindi wa pili Mamlaka za maji tuzo za NBAA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imekuwa mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.

Tuzo hizo zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zimefanyika juzi  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa DAWASA CPA, Sais Kyejo amesema imekuwa ni mara ya kwanza kushiriki katika tuzo hizo na wamefanikiwa kushika kwenye nafasi ya pili.

Kyejo amesema, kushika kwa nafasi hiyo kunaonesha wahasibu wanajua  kazi wanayofanya na wanazingatia viwango.

“Kupata kwa tuzo hii kuna maana kubwa sana kwa taasisi yetu sambamba na wahasibu waliopo kwenye idara ya fedha, tumeshiriki kwa mara ya kwanza, na tumeweza kufanya vizuri na hili linaleta chachu katika taasisi yetu na idara nzima,” amesema, wanaahidi kuendelea  kuwa katika Viwango bora kila siku kwani kupata kwa tuzo hiyo kumeleta chachu kwenye taasisi na idara nzima.

Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja aliweza kupokea tuzo hiyo ya mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles