30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC, TANESCO watakiwa kurejesha mali zinazomilikiwa na watu binafsi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said, ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Petrol na Gesi Tanzania (TPDC) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufuatilia na kurejesha mali zake zote zinazomilikiwa na watu binafsi zikiwemo za serikali.

Agizo hili linakuja baada ya TPDC kuendesha kampeni ya kurejesha mali zilizo kuwa zinamilikiwa na makampuni mbalimbali yaliyokuwa yameingia mikataba na shirika hilo, kutokana na muda wao kuisha kulingana na masharti ya makubaliano ya ubia huo,ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli.

Mhandisi Zena alitoa agizo hilo juzi wakati akikagua nyumba na kiwanja, maeneo ya Msasani Peninsular Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, vilivyo rejeshwa na kampuni ya Sheli ya Tanzania (Shell Petrolium Development Tanzania limited) vilivyo chukuliwa kwa makubaliano 1981.

“Ziko mali nyingi za serikali ambazo zinamiliki na watu binafsi,kinyme cha taratibu na sheria, hivyo zinatakiwa kurejeshwa haraka iwezekanavyo kwa serikali kama ilivyo agizo la Rais Dk. John Magufuli, lakutaka kurejeshwa kwa mali zote zilizotaifishwa na watu binafsi ambazo ni mali halali ya serikali.

“Ziko mali na fedha nyingi ambazo zinapotea bure na kutumiwa tu na makampuni ya watu binafsi ambayo yalitakiwa kuingizia serikali mapato kwa ukuaji wa uchumi lakini watu wameyataifisha,”alisema Katibu Zena.

Katibu huyo aliwataka watu wote na makampuni yote yanayo endeleza shughuli zakde kinyume nchini kinyume cha taratibu nasheria, kuhakikisha wanarudisha haraka mali hizo kwani, hata wakijificha hawata kaasalama watabainika tu kwa ukaguzi unaofanywa sasa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TPDC, Dk. James Mataragio alizitaka kampuni zote zilizomaliza makubaliano kurejesha mali zote kwa kampuni hiyo kama yalivyokuwa makubaliano ya mkataba yao.

“kwa mujibu wa mikataba yetu kwa makampuni  tuliyoingia nayo ubia,muda wake ukimalizika malizote watakazo zinunua na kuzinjenga ikiwa ni majengo na viwanja mara baada ya mkataba kuisha muda wake, zinarejeshwa mikononi mwa TPDC na itaziendeleza yenyewe,” amlisema Dk. Mataragio.

Aidha, Dk. Mataragio alisema kuwa malizote walizopokea kutoka kwa kampuni ya mafuta ya Shell, ambayo ni kiwanja na nyumba watajenga nyumba za watumishi wa shirika hilo na kuyaendeleza kwa shughuli zingine.

Pia, Katibu Zena, alifanya ukaguzi wa mradi wa gesi wa Kinyerezi katika kampuni tanzu ya gasco, ambapo alipongeza vijana wazawa ambao wamesaidia ukarabati wa mradi huo.

“Tunajivunia vijana wetu Watanzania wazawa, waliopo kwenye ujenzi wa mradi huu, kwani wamesaidia  katika mradi huo, hivyo wamesaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zinapotea kwa kulipa makampuni ya nje yaliyokuwa yanalipwa fedha nyingi,” alisema Katibu huyo.

Aliongeza kuwa mpaka sasa gesi inachangia kwa asilimia 60 ya umeme unaopatikana nchini.

“Tunayo maligahafi kubwa ya gesi  iliyovumbuliwa hapa nchini, ambayo ikikamilishwa itaondoa changamoto ya umeme iliyopo nchini, mbali na kuondoa changamoto hiyo ya uhaba wa umeme nchini, itapaisha zaidi pato la taifa kufikia malengo ya uchumi wa kati wa juu,” alisema Mhandisi Zena.

Pia alisema kukamilika kwa miradi  mikubwa ya gesi kama ule wa Julias Nyerere unaojengwa katika bwawa la mto rufiji, itasaidia kuondoa changamoto ya umeme nchini pamoja na kuongeza pato la taifa kwa kuuzia nchi jirani 

“Zipo nchi jirani ikiwemo Kenya na Uganda zimeshatuma maombi ilikupelekewa gesi hivyo itasaidia kukuza uchumi wetu.

“Tuna malighafi ya gesi hapa nchini ambayo imevumbuliwa hapa, maeneo ya baharini lakini tunaendelea kuifanyia utaratibu mbalimbali ilikuweka mikataba mizuri, itakayokuwa na tija kwa taifa letu isiyo ya kinyonyaji kama ilivyo dhamira ya Rais Dk.Magufuli,” alisema,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles