Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM.
SERIKALI imesema inahitaji kuugwa mkono usio na masharti ambao hautasababisha kumomonyoka kwa umoja na mshikamano wa Taifa na hivyo kusababisha machafuko na mvurugano wa amani.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen Mbundi katika mahafali ya 23 ya Chuo cha Diplomasia.
Alisema Taifa linahitaji vijana wasomi kutetea maslai ya nchi kwa kutumia elimu.
“Vijana wasomi wanatakiwa kutetea maslai ya nchi kwa kutumia elimu na uwezo wao katika kupambana na propaganda za wasio itakia mema nchi yetu ya Tanzania,”alisema
Aidha aliongeza kuwa Taifa lipo katika ukombozi wa kiuchumi katika ushindani wa kibiashara.
Hivyo amewataka wahitimu hao kujielekeza katika Diplomasia ya kiuchumi, ambayo itasaidia wananchi kukuza uwezo wa ushindani katika masoko kwa kuongeza uzalishaji wenye tija katika bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za kilimo na madini.
Hundi amewataka wanafunzi wanaohitimu katika chuo vha Diplomasia kuwa wabunifu na kuitumia vizuri elimu waliyoipata kutetea maslahi ya nchi yao.
“Licha ya chuo kuwa kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa eneo chuo kinaweza kuweka mpango mkakati unaoendana na matumizi ili kutatua changamoto hizo.” alisema
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Dk Abdulrahman Kaniki, alisema kuwa wahitimu waliotunikiwa vyeti katika mahafali ya 23, 2020 ni 667.
Alisema udahili kwa mwaka wa masomo 2020/2021 ameongezeka kutoka wanafunzi 834 kwa mwaka 2019, na kufikia wanafunzi 1130.
“Chuo kina changamoto ya ufinyu wa eneo hivyo uongozi wa Wilaya ya Pangani, wametupa hekari 50 ili kuweza kupanua huduma zetu na kufikia watu wengi zaidi”alisema Balozi Kaniki