25 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

NEC yaanika changamoto za Uchaguzi Mkuu 2020

Ramadhani Hassan, Dodoma

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezitaja changamoto ilizokutana nazo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ikiwemo  ya wasimamizi wa uchaguzi kutishwa na wagombea   kwa njia ya  simu na baadhi ya wagombea kukataa kushuka kwenye majukwaa wakati wa kampeni.

Hayo yalielezwa  jana Jijini hapa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya hiyo, Dk.Wilson Mahera  wakati akifungua kikao cha tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kikao hicho kilihudhuriwa na waratibu wa uchaguzi wa mikoa na wasimamizi wa majimbo yote nchini.

Mkurugenzi huyo alisema walikutana na changamoto nyingi kipindi cha uchaguzi ambazo ni pamoja na  wasimamizi wa uchaguzi kutishwa na wagombea kwa njia ya simu.

“Lakini kulikuwa kuna changamoto  ya vitisho, wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wakitiswa kwa simu, kuanzia ngazi ya majimbo hadi taifa lakini tunashukuru Mungu jambo limeisha,”alisema Mkurugenzi huyo.

Alizitaja changamoto nyingine ni pamoja na baadhi ya vyama vya siasa kutozingatia maadili ya uchaguzi,kuingilia ratiba za wengine,wagombea kupitisha muda wa saa 12 jioni.

“Mtu anakataa waziwazi anaambiwa shuka anasema sishuki lakini nawapongeza askari kwa kuchukua hatua sasa hayo yamepita,”alisema.

Pia alisema baadhi wagombea walikuwa hawatii maagizo ya kamati ya  maadili.

Kwamba walipokuwa wakiitwa walikuwa hawafiki.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu  pia mapingamizi mengi tofauti na chaguzi nyingine.

“Pia kulikuwa na pingamizi za kutosha sijui ni kwa sababu ipi? lakini nyingi zilikuwa wagombea kwa wagombea ilituletea shida kupitia na rufaa zilikuwa nyingi. Hoja ambayo inabidi tuingalie sana je ni watu kukosa elimu ya wapiga kura ama la,”alisema.

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo alisema uchaguzi wa mwaka huu umeendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria.

Vilevile, alisema uchaguzi wa mwaka huu kulikuwa kuna mawakala wengi ndio maana waliongeza siku kadhaa kwa ajili ya viapo.

Kwa upande wa watazamaji alisema kulikuwa na asasi 97 za ndani na  17 za Kimataifa huku jumla ya watazamaji  3297 walishiriki kutazama uchaguzi huo na  kuandika ripoti zao.

Alisema uchaguzi huo ulikuwa na watazamaji zaidi ya  5400 na hakuna ambaye alizuiliwa.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwa sababu mlikuwa wepesi kukusanya matokeo lakini mlikusanya kwa wakati na tulishirikiana vizuri na watu wa tehama.

“Hakika zile sifa za kutangaza matokeo ndani ya saa 48 tunazirejesha kwenu yote haya kwa sababu tulikuwa tunafanya kwa pamoja,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles