Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM
HOSPITALI binafsi ya Saifee iliyoko jijini Dar es Salaa imeanza kutoa huduma ya upasuaji wa moyo ili kusaidia kupanua huduma na matibabu hayo hapa nchini.
Hospitali Hiyo ni ya kwanza ya binafsi kuanza kutoa huduma hiyo hapa nchini mbali na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI).
Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum wakati wa vipimo vya magonjwa yasiyoambukiza yaliyomalizika mwishoni mwa wiki hii Afisa habari wa Hospitali hiyo Christina Manongi alisema wanatarajia kutoa huduma nzuri kwaaji ya afya ya wananchi.
“Katika viwanja hivi tangu tuanze vipimo mwitikio ni wa watu kuja kupima pasha na moyo ni mkubwa japo mvua zilitokea lakini watu walijitokeza bila kujali .
“Hapa tunatoa huduma za kipimo cha ICG kinaangalia umeme kwenye moyo ,tunapima kisukari pamoja na uzito ni muhimu sana kupima uzito watu wengi hawafahamu kuna kitu kinaitwa BMI hii ni muhimu sana kupima kwasababu pale unaangali urefu wako na uzito kama unaendana na kama haziendeni ni moja wapo ya hatari ya kuwa na uzito mkubwa ambao unaweza kusababisha presha na baadaye magonjwa ya moyo lazima tupime tuangalie hili,’’ alibainisha.
Alisema hospitali hiyo pia inatoa ushauri kuhusu masula ya lishe ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
“Wataalamu wakimpima mtu wanampa ushari kama kuna vyakula anatakiwa kuacha basi atashauriwa kufanya hiyo ili kuweza kunusuru afya yake.
“Vipimo vinachukua gharama Sh 30,000 na tunaendelea kuboresha ili kuwa na huduma nzuri zaidi nchini,”alisema Manongi.