25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Lowassa achangisha Sh milioni 300 ujenzi wa Kanisa

Na JANETH MUSHI – ARUSHA

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa Kuu (Cathedral) la KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati, ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba waumini 1,700.

Katika shughuli hiyo ya harambee iliyofanyika jana katika Usharika wa Mjini Kati-Kanisa Kuu, Lowassa alifanikisha kuchangisha zaidi ya Sh milioni 326.5, ambapo makisio ya kanisa hilo yakiwa ni kukusanya Sh bilioni moja.

Lowassa aliongoza harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa jengo hilo ambalo litajumuisha Kanisa na jengo la utawala na Sh bilioni 11 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk. Solomn Massangwa, alisema katika mradi huo Sh bilioni tisa zitatumika kwa ajili ya jengo la Kanisa Kuu pamoja na Sh bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala na mradi huo unatarajiwa kuanza Disemba mwaka huu na kukamilika baada ya miaka minne.

“Mradi huu ni muhimu kwani utaonyesha uso wa Dayosisi yetu na tumeona kuna umuhimu wa kufanya ujenzi kwa upya kwani la zamani halionyeshi hadhi kamili ya Dayosisi yetu na halitoshelezi pia,” alisema.

Aidha, kiongozi huyo wa Kanisa alitumia nafasi hiyo kuwatoa hofu baadhi ya waumini ambao walionekana kuwa na hofu ya kusema hadharani kiwango cha michango yao waliyotoa kwa ajili ya harambee hiyo ambapo wengine hawakuweza kuhudhuria kwa sababu ya hofu hiyo.

“Kwa wale ambao wamekuwa na hofu ya kutaja kiasi ambacho wanatoa, niwatie moyo wasiwe na wasiwasi kwa sababu hakuna mtu atakayewafuatilia. Ni vizuri na Wakristo tunapaswa kuwa huru, kama mtu unajua unadaiwa na Serikali, ulipe kodi ya Serikali usiwe na wasiwasi.

“Niwatoe hofu washarika na wananchi kwa ujumla, kuchangia maendeleo ya Kanisa ni muhimu na kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kulipa kodi ni jambo la msingi, kwa sababu hata Yesu alifundisha wanafunzi wake kuwa ya kaisari mpeni kaisari na ya Mungu mpeni Mungu,” alisema.

Kuhusu mwamko wa uchangiaji, Dk. Massangwa alisema wameuona mwamko tofauti na walivyotazamia awali kutokana na wengine kulalamikia hali ya uchumi kuwa siyo nzuri huku wengine wakihofia kuchangia.

“Nimshukuru Waziri Mkuu wa zamani, Lowassa kwa moyo wake wa kujitoa, amekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya Kanisa letu la KKKT, Mungu azidi kumbariki na viongozi wengine wawe tayari kujitoa kwa

ajili ya kazi na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” alisema.

LOWASSA

Katika harambee hiyo, Lowassa alichangia Sh milioni 20, huku familia yake ikichangia Sh milioni 17 ambapo aliwaomba waumini na wageni waliohudhuria harambee hiyo kuwa licha ya dunia kukumbwa na janga la corona lakini bado wana nafasi ya kuchangia maendeleo ikiwemo ya Kanisa.

“Watu wengi wanalalamika, uchumi wa dunia umeharibika kwa sababu ya janga hilo lakini Mungu aliyetulinda na janga hilo lazima tufanye kazi yake kwa kuunga mkono katika katika hili.

“Tumepewa kibali cha kuifanya kazi hii ya bwana,tuifanye kwa kushirikiana na nimpongeze Dk. Massangwa kwa kujitoa, uaminifu na asife moyo, ndiyo maana tumekuja kuwaonga mkono kwani hata Roma haikujengwa siku moja, msiogope tuifanye kazi hii.

“Nilipoalikwa katika shughuli hii nilisita, Kanisa gani hili limetoka kwenye mgogoro (corridor spring), lakini pili Kanisa gani halisikii kinachoendelea duniani (janga la corona), maswali ni ya msingi ila Mungu ametulinda,” alisema.

Aidha aliitaka Dayosisi hiyo kuhakikisha wanafuatilia vibali kwa ajili ya kuanzisha vituo vya redio na Tv mkoani hapa.

MWENYEKITI WA KAMATI

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kanisa hilo, Darius Dipa, alisema sababu kubwa iliyowalazimu kuanza ujenzi wa Kanisa jipya ni kutokana na Usharika huo kutambuliwa kuwa Kanisa Kuu la Kiaskofu katika Dayosisi hiyo, hivyo Kanisa lililopo sasa kuoneakana kutokidhi viwango.

Alisema Kanisa hilo lenye uwezo wa kuketisha waumini 1,700 kwa wakati mmoja litakuwa la kisasa likiwa na viti 100 vyenye vifaa maalum vya kuvaa masikioni kusikia tafsiri ya lugha pindi wanapokuwa na wageni bila kutumia mkalimani.

“Kutakuwa na chumba cha habari, chumba maalum cha kunyonyeshea watoto, viti vya kisasa, huku tukizingatia suala la walemavu na wazee,” alisema.

Alisema kutoka na ufinyu wa eneo, ujenzi utaanzia chini ya ardhi kwa ghorofa mbili zenye uwezo wa kuegesha magari 270 kwa wakati mmoja na kuwa kazi iliyopo kwa sasa ni kuondoa majengo ya zamani isipokuwa Kanisa linalotumika kwa sasa kwa ajili ya ibada.

Mwenyekiti huyo alisema wanatajia kuanza ubomoaji na uchimbaji wa eneo kuanzia Desemba 8 mwaka huu na kuwa mchakato wa kumpata mkandarasi kwa njia ya zabuni ulishafanyika na kumpata Mkandarasi ambaye ni

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles