25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

NGO’s zajipanga kuendana na dira ya serikali

 Na JANETH MUSHI
-ARUSHA

MBUNGE wa Viti Maalum anayewakilisha kundi la Asasi za Kiraia (NGO’s),Tanzania Bara,Neema Lugangira amesema atahakikisha asasi zisizo za kiraia,mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wadau wa maendeleo wanatekeleza mambo ambayo yanaendana na dira ya serikali.

Akizungumza na MTANZANIA jana,amesema baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Dk.John Magufuli,wakati wa uzinduzi wa Bunge la 12,binafsi ameona nafasi yake ya kuchangia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya CCM pamoja na dira ya serikali na kuwa masuala mengi yanayofanywa ngazi ya jamii yanafanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia.

 “Tayari binafsi naiona nafasi yangu ya kuchangia kwa ukamilifu kwenye utekelezaji wa dira aliyotupatia Rais na mimi kama mwakilishi wa kundi hilo naamini nahitaji kuzitambua kwenye maeneo haya ya kipaumbele wanafanya nini na wadau wa maendeleo wanafadhili maeneo gani,je yanaendana sambamba na dira ya serikali?

Aidha alipongeza mpango mkakati wa serikali kuboresha mazingira wezeshi ya biashara kwa nia thabiti ya kuongeza uwekezaji ambao utapelekea kuongeza ajira mbalimbali.

“Hotuba ya Rais nimeisikilzia nimefarijika sana kwa sababu amegusia kikamilifu sekta ya kilimo na umuhimu wa kuiunganisha sekta hiyo,mifugo na uvuvi pamoja na sekta binafsi,”

“Lakini sambamba na hilo nimefarijika kuona namna amegusia makundi ambayo mimi binafsi ni makundi yangu ya kipaumbele ikiwemo uwezeshaji uchumi wanawake,mikopo isiyokuwa na riba kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu,”anasema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles