25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kinondoni wataka wananchi kuondoka vituoni wakishapiga kura

Salome Bruno na Nasra Hussein (TUDARCO)

KAMANDA wa Polisi Kinondoni, Edward Bukombe, amewataka wananchi kuzingatia taratibu na sheria za Uchaguzi Mkuu wakati wa kupiga kura Oktoba 28 ili kuepusha vurugu na kwamba wakimaliza kupiga kura waondoke kwenye vituo vya kupigia kura.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano na waandishi wa habari.

“Jeshi la polisi linatoa rai kwa wananchi kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi katika kipindi hiki cha uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28 ili kuepuka uvunjifu wa amani, wote watakaokinzana na sheria hatutasiata kuwachukulia hatua kali za kisheria. Wananchi wote wanaagizwa kuondoka kwenye vituo mara tu wanapomaliza kupiga kura,” alisema.

Katika hatua nyingione, alisema jeshi hilo limefanya operesheni za kusaka wahalifu wanaojihusisha na matukio mbalimbali kama vile wezi wanaotumia bodaboda kupora watu (vishandu), kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi wa pikipiki na kupatikana na mali za wizi na wizi .

Alisema Septemba 16 hadi Oktoba 16 katika maeneo ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, katika operesheni iliyofanyika maeneo ya Masaki, Kimara, Ubungo, Kinondoni, Makongo, Goba na Mwananyamala, lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 30 kwa tuhuma za wizi na walionunua mali za wizi.

Alisema katika operesheni hiyo, walikamata pikipiki tano aina ya boxer zenye namba za usajili MC.866 BQC , MC.898 CNG , MC.978 CKK , MC.151 CDH, MC.659 BVX , gari namba T.240 DSX aina ya Toyota IST inayotumika kufanya uhalifu.

Alisema pia walikamata televisheni 22, kompyuta mpakato moja aina ya lenovo nyeusi, friji moja aina ya hoeva, meza moja, viti sita, mabati 15 mapya,  mashine ya kufulia nguo moja, taa za kamera za ulinzi nne, feni mbili, jagi la kuchemshia maji moja, vifaa vya kutengenezea pikipiki, kinanda, simu na pesa Sh milioni  2 .8.

“Jeshi la polisi linatoa taarifa kwa wananchi ambao wameibiwa mali zao waweze kufika kituo cha polisi Oysterbay wakiwa na stakabadhi halali ili waweze kutambua mali zao,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles