24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jela miaka miwili kwa kuua mke bila kukusudia

Kulwa Mzee , Dar es salaam

MKAZI wa Dar es Salaam Yusuph Ismail (45), aliyekaa mahabusu miaka saba amehukumiwa kwenda jela miaka miwili, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua mkewe bila kukusudia.

Mshtakiwa huyo alitiwa hatiani jana na Mahakama Kuu iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Mshtakiwa anadaiwa kumuua mkewe kwa kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumyonga wakati wote wakiwa wamelewa pombe kwa madai ya kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yake.

Akisoma hukumu hiyo  Hakimu Shaidi, alisema mshtakiwa anamhukumu kutumikia kifungo cha miaka  miaka miwili jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia ambalo alikiri.

“Inaonyesha mshtakiwa na marehemu mlikuwa na ugonvi mara kwa mara na ni kwasababu ulikuwa unamtuhumu kuwa alikuwa sio mwaminifu, mshtakiwa ulitumia misuli mingi kwa mtu ambaye hana nguvu hizo, ukamuua mkeo kwa kumyonga,” alisema.

Hakimu Shaidi, alisema kwakuwa mshitakiwa alikaa ndani tangu mwaka 2013 kwa kuzingatia hilo mahakama inampunguzia adhabu ambapo ni miaka miwili jela.

Kwa upande wa Wakili wa Serikali Ashura Mnzava, aliomba mahakama kumpa mshitakiwa adhabu stahiki ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wanafanya ugonvi wakiwa wamelewa.

 Naye Wakili wa Utetezi, Themistocles Rwegasira, aliomba mahakama impunguzie adhabu mshitakiwa kwakuwa alitoa ushirikiano kwa polisi, hakukana kosa na hajaisumbua mahakama.

“Kitendo hicho kilitokea wote wakiwa wamelewa, mshtakiwa ndiye alikwenda kutoa taarifa kwa majirani baada ya pombe kumtoka, hivyo naomba mahakama impunguzie adhabu, amekaa ndani tangu mwaka 2013,” alidai.

Kabla ya mshtakiwa kusomewa hukumu hiyo, alikumbushwa mashitaka yake ambapo alikiri kosa hilo na kisha kusomewa maelezo ya awali.

Akisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava, alidaiwa mshtakiwa pamoja na marehemu walikuwa mke na mume wakiishi Tegeta A, Dar es Salaam ambapo wakati wa maisha yao walikuwa na mikwaruzano iliyosababisha kugombana mara kwa mara.

Novemba 17 mwaka 2013 marehemu Magdalena Fabian au Maria alirudi nyumbani kwake baada ya kupotea siku kadhaa akiwa amelewa.

Marehemu baada ya kuhojiwa na mumewe kwamba alikuwa wapi hakukuwa na maelekezo ya kujitosheleza, hivyo mshitakiwa alianza kumpiga marehemu kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mwishowe alimyonga hadi kufa.

Mshtakiwa baada ya tukio hilo alimbadilisha nguo marehemu ambazo zilikuwa na damu na kinyesi kabla ya kutoa taarifa kwa majirani.

” Mshtakiwa alikwenda kwa jirani pamoja na mjumbe wa nyumba 10 kwamba ameamka asubuhi na kukuta mwili wa marehemu akiwa amefariki dunia kitandani.

“Baada ya taarifa hizo majirani pamoja na mjumbe alifika eneo la tukio na kisha kuripoti kituo cha Polisi Kimara ambapo askari walifika na kuchukua mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Mwananyamara,” alidai

Wakili Ashura, alidai ripoti ya uchunguzi ilionyesha marehemu alifariki baada ya kuvuja damu nyingi itokanayo na majeraha ya maumivu.

Kutokana na tukio hilo mshtakiwa alikamatwa na baada ya kuhojiwa alikiri kumyonga mkewe hadi kufa ambapo mshitakiwa alifunguliwa mashitaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles