32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawaonya waajiri

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema waajiri wote nchini wanawabijika kutekeleza na kuzingatia sheria za kazi na hivyo kuwataka waache kupotosha.

Taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama  ilieleza kuwa katika siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya waajiri wasiozingatia Sheria za Kazi kwa makusudi kwa kisingizio kwamba hawawajibiki chini ya Sheria hizo. 

“Waajiri hao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa Maofisa Kazi wanapotekeleza majukumu ya kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi katika maeneo ya kazi. 

“Aidha, waajiri hao wamekuwa wakitoa taarifa potofu kwa Umma, Viongozi wa Serikali na Wanajumuiya wao kwa lengo la kudhoofisha juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa Sheria za Kazi zinafuatwa na kuzingatiwa nchini,” ilieleza taarifa hiyo.

Jenista alisema anawakumbusha na kuwasisitiza waajiri wote kwamba wanapaswa kuzingatia na kutekeleza matakwa ya Sheria za Kazi.

“Ninatoa rai kwa waajiri wote nchini kutoa ushirikiano kwa Maafisa Kazi wanapotekeleza majukumu yao ya kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi,” alisema. 

Alisema iwapo kuna changamoto yoyote katika utekelezaji wa Sheria, waajiri wawasiliane na Ofisi yake badala ya kutoa taarifa potofu kwa Umma, Viongozi wa Serikali na Wanajumuiya wao.

“Ninaomba kuwahakikishia waajiri wote kuwa, Serikali yetu inathamini Sekta zote ikiwemo Sekta Binafsi na Sekta ya Umma pamoja na Uwekezaji unaofanywa nchini kwa ustawi wa Taifa letu” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles