22.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

TMDA yakana dawa hizi

Na  AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) imekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwepo kwa dawa za Covifor na Jubi-R  hapa nchini  ambazo zinatajwa kutumika katika matibabu ya Covid-19.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa TMDA, Adam Fimbo ilisema kuwa dawa hizo bado hazijasajiliwa  kwaajili ya matumizi. 

“Hivi karibuni  kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikihusisha dawa zenye kiambata hai (active ingredient) kinachofahamika kwa kitaalamu kama Remdesivir ambacho kimegundulika  kuwa na uwezo  wa kutibu ugonjwa wa Covid -19.

“Dawa hizo zenye viambata hai hiki zinajulikana kwa majina ya kibiashara kama Covifor inayotengenezwa na kampuni  yenye jina Hetero Labs Ltd   na Jubi-R  inayotengenezwa na Jubilant Generics Ltd zote za nchini India.

“Dawa hizi za sindano zimefungashwa kwenye kifungashio ambacho lebo zake  zinaonesha haziruhusiwi kusambazwa kwa nchi za Marekani ,Canada na Umoja wa Ulaya ambapo maandishi hayo yameleta taharuki  na wasiwasi  kwamba inawezekana  dawa  hizi zinazosambazwa maeneo mengine sio salama au duni na hazifai kwa matumizi yaa binadamu.

“Hivyo mamlaka inapenda kutoa ufafanuzi  uandishi wa  maneno hayo kwenye lebo ni wa kawaida  kwenye sekta ya dawa ,”alibainisha.

Alisema kuwa lengo la maneno hayo ni kuzuia  usambazaji wa dawa hizo kwenye nchi mbazo mtengenezaji  au mgunduzi  wa kwanza  hajaruhusiwa  kutokana na kuweka hakimiliki ya dawa yake.

“Dawa hii ya Redemsivir imegunduliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya jina la Gilead Ltd iliyoko nchini Marekani  na imesajiliwa kwa dharura  na mamlaka ya udhibiti wa dawa  na chakula  nchini Marekani(US-FDA)  kwaajili ya kutibu Covid-19.

“Utaratibu huu unatumika kuidhinisha na US-FDA kwa  dawa ambazo tafiti zake hazijakamilika  ipasavyo kabla haijaruhusiwa rasmi  kutumika kwa binadamu  ili kuzuia na kutibu  magonjwa yanayoambukiza kwa kasi na kusababisha vifo  ikiwa kama hamna dawa nyingine  kama ilivyo kwa Covid-19,Ebola  na mengine.

“Kwa mantiki hiyo dawa zilizotajwa hapo juu zinatengenezwa na makampuni hayo mawili  ya India  baada ya kupewa kibali maalum na kampuni ya Gilead Ltd  kwaajili ya kutengeneza dawa za genesi  ili ziweze kutumika kwenye nchi zingine 127 duniani  kwa mujibu wa makubaliano  tofauti na nchi za Marekani,Canada na EU,”alifafanua. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,647FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles