27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lundo la mitihani lawasubiri wanafunzi Kenya

NAIROBI, KENYA

SERIKALI ya Kenya inapanga kusimamia mitihani ya tathimini ya kitaifa kwa watoto wote wa shule za msingi wakati shule zitakapofunguliwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa jana na gazeti la The Standard nchini humo, mitihani hiyo ni kwa ajili ya kufanya tathimini kupima uelewa wao baada ya miezi kadhaa ya kufungwa shule kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona.T

Kwa mujibu wa The Standard imebaini kwamba tayari Baraza la Taifa la Mitihani nchini Kenya (Knec) linaandaa mpango wa kufanya tathimini hiyo ambao utapelekwa katika shule zote kufahamu tabia za watoto kujifunza kabla ya masomo kuanza.

Tathmini zote zitafanywa shuleni ambapo walimu wataweka alama na kuzituma Knec.

Shule bado zimeendelea kufungwa nchini Kenya tangu Machi wakati kisa cha kwanza cha mgonjwa wa corona kiliporipotiwa na Waziri wa Elimu George Magoha amekwua akishutumiwa kutoa ishara tofauti tofauti kuhusu kufunguliwa shule.

Jumanne wiki hii, Magoha  alisema uamuzi wa iwapo shule zitafunguliwa utatangazwa baada ya mkutano mkuu wa wadau unaotarajiwa kufanyika Septemba 25 au kabla.

Theluthi mbili ya watoto duniani kote wamekwama nyumbani kutokana na virusi vya corona.

Kwa mujibu wa mpango huo, shule zitapewa sapoti ya kuchapisha na kusimamia tathimini hiyo.

Mpango huo ni sehemu ya shilingi za Kenya bilioni 1.5 zilizotolewa na Global Partnership for Education (GPE) kwa ajili ya kuzisaidia shule za serikali maandalizi ya kufunguliwa.

Tume ya walimu, na taasisi ya mitaala ya elimu  pamoja na Knec zinatarajiwa kufaidika na fedha hizo ambazo zitaratibiwa na Benki ya Dunia.

Kwa mujibu wa mpango  huo  ambao umependekezwa na Knec, tathini kwa watoto wa darasa la kwanza hadi sita  itafanywa kwa kuaangalia misingi ya masomo, namba,hesabu, kusoma na kuandika sayansi na lugha.

Wanafunzi wa darasa la saba na nane watafanyiwa tathimini kupitia masomo ya KCPE.

Mapendekezo kama hayo yapo pia kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari  kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne.

Knec imesema mpango huo una lengo la kuwasaidia walimu kufahamu kiwango cha uelewa cha wanafunzi  na matokeo yake hayatatumika kuwapanga watoto kimadaraja au kuamua kupita madarasa ya juu. 

Maelezo kamili yanafunua kwamba wanafunzi wote wa Daraja la Kwanza hadi la Nane katika shule zote za msingi za umma na za binafsi  watalengwa na tathmini hiyo.

Kwa mujibu wa mpango huo, darasa la kwanza hadi la tatu watafanyiwa tathimini kwenye namba, kusoma na kuandika, wakati darasa la 4,5 na sita watajaribiwa kwenye hesabu, lugha na sayansi.

“Katika Daraja la 4, Mahitaji Maalum  Elimu (SNE)  ya kuvuka darasa pia yatatathminiwa,” linaeleza andiko la Knec.

Kaimu Ofia Mtendaji wa Knec, Mercy Karogo jana alisema kuwa majaribio hayo yatafanywa kwa muda kwa ajili ya kuwasaidia watoto kwenye masomo yao ili kufidia muda waliopoteza.

“Walimu wataweza kutathmini viwango vya uelewa wa watoto katika darasa lao na kuagiza njia bora za kuwasaidia kufidia  muda uliopotea,” alisema  Karogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles