LONDON, UINGEREZA
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ameongeza shinikizo kwa Umoja wa Ulaya muda mfupi kabla ya kuanza duru nyingine ya mazungumzo ya Brexit.
Johnson ameutaka Umoja wa Ulaya (EU) kutoa ushirikiano katika mazungumzo yajayo ya Brexit akiweka muda wa mwisho wa kufikiwa makubaliano ni Oktoba 15.
Juzi Shirika la Habari la Press Association, limeripoti Johnson alisema itakapotokea hakutapatikana makubaliano pia yatakuwa matokeo mazuri kwa Uingereza katika matamshi ambayo yangetokea jana, atauambia Umoja wa Ulaya iwapo makubaliano hayatafikiwa katika mkutano na Baraza la Ulaya Oktoba, pande zote mbili zinapaswa kujitayarisha kukubali hilo na kuendelea na shughuli nyingine.