24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Guterres: Watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu

NEW YORK, Marekani 

KATIBU Mkuu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa kushikamana na kuchukua hatua zinazohitajika dhidi ya hewa chafu inayovutwa na watu 9 kati ya 10 kila uchao duniani kote.

Gutarres aliyasema hayo jana kupitia ujumbe wake wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya bluu, ambapo alionya kuwa hewa chafu inayovutwa inachangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya moyo, kiharusi, saratani ya mapafu na magonjwa mengine ya mfumo wa hewa. 

“Inasababisha takribani vifo milioni 7 visivyo vya lazima kila mwaka hususan nchi za kipato cha chini na cha wastani. Uchafuzi wa hewa pia unatishia uchumi , uhakika wa chakula na mazingira,” alisema Gutarres.

Alisema wakati wakati huu ambao dunia inajikwamua kutoka kwenye janga la ugonjwa wa corona,inapaswa kutoa msukumo mkubwa kuhusu suala la uchafuzi wa hewa ambao pia unaongeza hatari zinazohusiana na COVID-19.  

 “Lazima pia tushughulikie haraka tishio kubwa la mabadiliko ya tabianchi, kuhakikisha ongezeko la joto duniani linasalia nyuzi joto 1.5 hali ambayo itasaidia kupunguza uchafuzi wa hewa, vifo na magonjwa,” alisema.

Akitoa mfano, alisema mwaka huu hatua za kudhibiti kusambaa kwa corona zilizolazimisha kufungwa kila kitu na watu kusalia majumbani zimesaidia kiwango cha hewa chafuzi kushuka kwa kiasi kikubwa na hivyo kutoa matumaini ya hewa safi katika miji mingi. 

Alionya  uchafuzi wa hewa tayari unaongezeka tena na katika baadhi ya maeneo zaidi  hata ilivyokuwa kabla ya COVID-19, 

“Kuliko wakati mwingine wowote sasa tunahitaji mabadilio makubwa na ya kimakati . Kusisitiza hatua za viwango vya mazingira, sera na sheria ambazo zinazuia wachafuzi wa hewa,” alisema/

Alizitaka nchi kuacha kutoa uzuku kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya kisukuku katika ngazi  kimataifa amezitaka nchi kushirikiana

ili kusaidiana kuingia katika teknolojia  za hewa safi. 

Alitoa wito kwa serikali mbazo bado zinafadhili miradi ya mafuta kisukuku katika nchi zinazoendelea kuelekeza ufadhili huo kwenye nishati safi na usafiri endelevu. 

Alizitaka nchi zote kutumia fungu la kujikwamua baada ya COVID-19 kusaidia kuunga mkono mabadiliko ya kuingia katika ajira zenye afya na ndelevu. 

Siku  kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya blu itaendelea kuadhimishwa kila Septemba 7 ya kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles