27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Pato la Taifa lafikia Sh trilioni 71.7

NBS-1Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

THAMANI ya pato la Taifa kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka kati ya Julai hadi Septemba 2015 imeongezeka hadi kufikia Sh trilioni 71.7.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa, alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 6.9.

“Pato la Taifa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka jana limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3, ikilinganishwa na asilimia 5.4 mwaka 2014. Hii inamaanisha Serikali imeondolewa kutoa huduma  mbalimbali kwa wananchi wake kama ilivyopangwa katika sekta zote za uchumi,” alisema.
Alisema thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi iliongezeka kwa asilimia 3.3 kutokana na mauzo ya dhahabu, almasi na madini mengine.

Dk. Chuwa alisema thamani ya bidhaa na huduma zilizoagizwa kutoka nje zilipungua kwa asilimia 0.58.

Alisema shughuli nyingine za uchumi zilizochangia pato la Taifa ni sekta ya ujenzi kwa asilimia 17.6, uchukuzi na uhifadhi asilimia 10.6, uendeshaji Serikali na ulinzi asilimia 10.6, wakati uchimbaji madini na kokoto vimechangia asilimia 8.0.

“Katika kipindi hicho shughuli za kilimo, uzalishaji viwandani, umeme, biashara za jumla na rejareja,  habari na mawasiliano, fedha na bima zilikua kwa kasi ya chini ya asilimia 3.0 ikilinganishwa na mwaka 2014.
“Kilimo cha mazao kilikua kwa asilimia 2.6 mwaka jana, ikilinganishwa na asilimia 3.1 mwaka 2014,” alisema Dk. Chuwa
Alisema uzalishaji wa bidhaa viwandani ulikua kwa asilimia 3.6, huku shughuli za fedha na bima zikichangia kwa asilimia 6.6.
“Kwa makadirio pato la Taifa linakadiriwa kufikia Sh trilioni 89.1 tangu Januari hadi Desemba, mwaka jana,” alisema.

Kwa upande wake, mtafiti wa masuala ya uchumi na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja, alisema jitihada zinahitajika ili Serikali ifikie lengo la kuinua uchumi wa wananchi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles