22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri atishia kuvunja Baraza la Wauguzi

Picha-na-1Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ametoa siku saba kwa viongozi walio chini yake kumwandikia sababu za kitaalamu zitakazomshawishi asivunje Baraza la Wauguzi Tanzania kwa kuwa limeshindwa kutimiza wajibu wake.

Waziri Ummy alitoa agizo hilo jana wakati alipokuwa akizungumza na wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo walifikisha malalamiko yao juu ya baraza hilo.

Wauguzi hao walilalamikia uongozi wa baraza hilo kuwa umeshindwa kudhibiti utitiri wa vyuo vinavyotoa elimu ya uuguzi hata kwa watu ambao hawajatimiza vigezo.

“Mmeniambia baraza hili limeshindwa kudhibiti utitiri wa vyuo na kusimamia mitaala yake itoe elimu ya uuguzi hadi kwa watu ambao wamepata daraja la sifuri.

“Ndiyo maana siku hizi watu hawana imani na wauguzi, wanaona heri wakatibiwe na mabibi zetu huko ‘tiba asili’, najua NACTE walipitisha mwongozo kwamba watoe elimu kwa ngazi ya cheti kwa miaka miwili, yaani sawa na uhasibu, hili ni jambo ambalo sikubaliani nalo.

“Katika hili ikiwezekana hata Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi aandikiwe barua kwa sababu NACTE walipitisha na ipo chini yake, mimi sikubaliani nalo… lazima fani ya uuguzi iheshimiwe,” alisema.

Aliwahakikishia wauguzi hao kuwa watasimamia suala la masilahi yao kuongezwa tofauti na ilivyo sasa.

Awali akisoma risala ya wauguzi, muuguzi Agnes Mtawa alisema wauguzi hao wamekuwa wakifanya kazi ngumu kiasi cha asilimia 70 kuugua migongo.

“Tunahudumia idadi kubwa ya wagonjwa wakati mwingine wanazidi, tunafanya kwa moyo tu, masilahi yetu bado ni madogo ikilinganishwa na kada nyingine ikiwamo ya madaktari,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles