29.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi waonywa kupiga watoto

Na ELIUD NGONDO, MBEYA

OFISA Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Theresia Mwendapole amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwapiga watoto na kuwanyanyasa kutokana na kuwapigia kelele wakiwa nyumbani kipindi hiki cha ugonjwa wa corona.

Hayo yalisemwa jana, wakati wa kikao cha baraza la madiwani kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwanyanyasa watoto hao na kuomba madiwani kuendelea kutoa elimu zaidi huko vijijini.

Alisema kutokana na vipigo, imekuwa changamoto wengi wao kushindwa kukaa nyumbani, badala yake wanazurura mitaani.

“Kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji kwa watoto hasa vipigo kipindi hiki cha corona, naomba wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mazuri na sio kuwapiga,” alisema.

Alisema wazazi na walezi, wanatakiwa kuwatafutia michezo ambayo itawafanya watoto wakae nyumbani kwa utulivu na sio kuwasumbua wao.

Diwani wa Kata ya Kambikatoto, Noah Mchafu (Chadema) alisema Serikali ya wilaya inatakiwa kuendelea kulisimamia suala hilo,licha ya kuwapo na unyanyasaji huo, pia kumekuwapo na mlundikano wa abili kwenye vyombo vya usafiri.

Alisema katika vyombo vya usafiri kumekuwapo na hali mbaya ambayo mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaweza kutofanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Mabasi yanayotoka mikoa ya Tabora na Singida, yanajaza abiria kiasi ambacho hali ya usalama wa watu ni mdogo, pale kwenye korido ya gari hakuna hali ya usalama kabisa,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Maryprisca Mahundi alisema jeshi la polisi linatakiwa kusimamia suala hilo ili kuhakikisha usalama wa Watanzania unakuwepo.

Alisema Serikali imetoa mwongozi wa kila gari la abiria kutozidishwa, lakini kumekuwapo na ukiukwaji wa makusudi kwa waendesha vyombo hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri, Bosco Mwanginde alisema madiwani wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha maagizo ya Serikali yanatekelezwa na sio kukaa kimya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles